1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Ethiopia yatangaza mazungumzo na waasi wa Oromo

24 Aprili 2023

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, amesema serikali yake imeanzisha mazungumzo na kundi la waasi lililoko katika jimbo la Oromia.

https://p.dw.com/p/4QV4M
 Ethiopia I  “Enough With War - Let’s Celebrate Peace” in Addis Ababa
Picha: Office of Prime Minister of Ethiopia

Taarifa hiyo ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na Jeshi la Ukombozi la Oromo, OLA ilitolewa siku ya Jumapili na waziri mkuu huyo ambaye alisema kuwa serikali na watu wa Ethiopia, wanayahitaji mno mazungumzo hayo. 

Jeshi la OLA limekuwa likipambana na serikali ya shirikisho ya Ethiopia tangu lilipogawanyika mwaka 2018 na chama cha kihistoria cha Oromo Liberation Front (OLF) kilipoachana na mapambano ya kutumia silaha.

Jimbo la Oromia lina idadi kubwa zaidi ya watu nchini humo na linauzingira mji mkuu, Addis Ababa.

Hapo jana Jumapili, Abiy alisema mazungumzo na Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA) yataanza Jumanne nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa serikali ya Ethiopia na Waethiopia wanahitaji mazungumzo hayo zaidi na hivyo ametoa wito kwa kila mhusika kutimiza wajibu wake.

Jeshi la OLA limekuwa likipigana na serikali ya shirikisho la Ethiopia, tangu lilipojitenga na jeshi la shirikisho mnamo mwaka 2018 na kutangaza mapambano ya silaha.