1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Ethiopia yatangaza hali ya dharura

4 Agosti 2023

Serikali ya shirikisho nchini Ethiopia imetangaza hii leo hali ya dharura kufuatia siku kadhaa za mapigano kati ya jeshi na wanamgambo katika eneo la Amhara.

https://p.dw.com/p/4Um8I
Äthiopien  | Bürgerkrieg
Picha: Amanuel Sileshi/AFP/Getty Images

Mapigano hayo yaliyozuka wiki hii katika eneo la pili kwa ukubwa nchini Ethiopia kati ya wanamgambo wa Fano na Jeshi la Ulinzi la Ethiopia, yamegeuka kuwa mgogoro mkubwa wa kiusalama.

Soma pia:Mkuu wa chama tawala Amhara auwawa

Jana, serikali ya Amhara iliomba msaada zaidi kutoka kwa mamlaka ya shirikisho ili kurejesha hali ya utulivu.

Hata hivyo taarifa hii ya ofisi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ya kutangaza hali ya dharura, haikubaini iwapo hatua hiyo itatekelezwa katika mkoa wa Amhara pekee au kote nchini Ethiopia.