1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yashinda mbio za nyika za dunia

31 Machi 2008

Wanariadha wake kwa waume wa Ethiopia wamewapiku wa Kenya katika mbio za nyika Scotland jana.

https://p.dw.com/p/DXwa

Wanariadha wa Ethiopia -Kenenisa Bekele , Tirnesh na Genzebe Dibaba wawapiku wakenya katika mbio za nyika za dunia huko Scotland.Harambee Stars (kenya)yailaza Taifa Stars -Tanzania bao 1:0 katika kinyan'ganyiro cha kombe la dunia .Bayern munich yaendelea kupepesuka katika Bundesliga baada ya kupoteza tena pointi kileleni katika changamoto za Bundesliga.

►◄

Kenya Harambee Stars na Taifa Stars ya Tanzania zilikutana mjini Nairobi jumamosi. kupimana nguvu . Harambee stars ,ilitambakwa bao 1:0 ,kocha wa Taifa Stars,mbrazil Maximo amewaonya Harambee wasishangirie na mapema ,kwani kuteleza si kuanguka kwa timu yake.

Katika Ligi mashuhuri za ulaya, klabu iliogonga vichwa vya habari mwishoni mwa wiki ni Energie Cottbus ambayo kwa ushindi wa mabao 2:1 dhidi ya Herzha Berlin imejikomboa kutoka safu ya timu 3 zinazoweza kushushuwa daraja ya pili msimu ujao.

Viongozi wa Ligi Bayern munich wamesalia hatahivyo kileleni licha ya kupoteza tena pointi 2 baada ya kumudu sare tu ya bao 1:1 na mahasimu wao wa kusini mwa Ujerumani Nüremberg.Ilikua chipukizi wao asieridhika nao,Lukas Podolski alieikoa Munich kwa kutia bao hilo la kusawazisha.

Baadae kocha wa Bayern Munich, Ottmar Hitzfeld alitupa jukumu la kushindwa kutamba kwa timu yake kumetokana na machofu ya wachezaji waliopata kati ya wiki pale Ujerumani ilipocheza na Uswisi:

Mstuko mkubwa katika Bundesliga ulikuja kwa werder Bremen iliozabwa mabao 2:1 na Duisburg.Schalke 04 inayocheza kesho katika robo-finali ya champions League

na FC barcelona mjini Gelsenkirchen,haikumudu zaidi ya sare ya 0-0 na Karlsruhe na pointi moja imewatupa nafasi ya 3 .Bayer Leverkusen imekiona cha mtema kuni kwa madhambi iliofanya wenyewe langoni mwao.Mshambulizi wao Stefan Kiessling aliutia kichwa mpira wavuni wakati akijaribu kuokoa.Mwishoe, leverkusen ilizabwa mabao 2:0 na Frankfurt.

Hamburg ilitoka sare bao 1:1 na Armenia Bielefeld.

Mechi 7 zikisalia katika serie A, kabla kumaliza msimu,AC Milan imeanza kupatwa na homa ya wasi wasi.Wakiwa nafasi ya 6 katika ngazi ya Ligi ya Itali,AC Milan imeshindwa mapambano yao 2 yaliopita nyumbani na iko nyuma ya Fiorentina katika ngazi ya Ligi.Msimu uliopita, AC Milan ikitamba.Ilitwa kombe la ulaya na halafu ikatawazwa mabingwa wa kombe la klabu bingwa ya dunia.Lakini msimu huu yaonesha kana kwamba, "ngoma ikivuma sana, haikawii kupasuka."

Katika La Liga, Ligi ya Spain ,Real madrid imeondoa shaka shaka zozpte zilizokuwapo kwamba kombe ni lao msimu huu.Na hilo litakua taji lao la pili mfululizo.Real ilikomea Sevilla mabao 3-1 kwa furaha ya kocha wao Bernd Schüster.Villareal imechukua nafasi ya pili ilipokua FC Barcelona b aada ya kuikomea Atletico Madrid jumamosi mabao 3-0.

Waethiopia walitamba jana huko Edinburgh Scotland katika mbio za nyika za ubingwa wa dunia: Kennenisa Bekele na Tirunesh Dibaba walizima vishindo vya kenya katika daraja zote waume na wanawake,wakubwa na chipukizi na kutoroka na mataj jumlai.Paul Tergat, bingwa mara 5 wa mbio za nyika, amewaonya wakenya wenzake kama hawatachunga Kenya, itapoteza usukani wa mbio ilizozidhibiti miaka mingi.