1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yaishutumu Marekani kwa taarifa zenye kubomoa

Sylvia Mwehozi
8 Desemba 2021

Ethiopia imeishutumu Marekani kwa kuendeleza taarifa zenye kutia doa nchi hiyo, baada ya Washington na washirika wake kuelezea wasiwasi juu ya watu kukamatwa kiholela kwa misingi ya ukabila.

https://p.dw.com/p/43z2a
Äthiopien | Premierminister Abiy Ahmed Ali
Picha: Office of the Prime Minister Ethiopia/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Shutuma za Ethiopia zinajiri kutokana na Washington na washirika wake kuelezea wasiwasi juu ya watu kukamatwa kiholela kwa misingi ya ukabila nchini Ethiopia.

Marekani na baadhi ya mataifa ya magharibi walitoa taarifa ya pamoja siku ya Jumatatu, raia wa Tigray wanakamatwa kwa wingi.

Serikali ya Ethiopia ilitangaza hali ya hatari ya nchi nzima mapema mwezi uliopita baada ya chama cha ukombozi wa watu wa Tigray TPLF kutangaza ushindi mkubwa katika barabara muhimu za kuelekea Addis Ababa.

Msemaji wa waziri mkuu Abiy Ahmed, Billene Seyoum amesema kuwa hatua hizo hazilengi kundi lolote la watu kwa kuzingatia ukabila.

Matamshi yake yametolewa saa chache baada ya serikali kutangaza kuidhibiti miji miwili ya kimkakati ya Dessie na Kombolcha.