SiasaEthiopia
Ethiopia na waasi wa TPLF kuunda chombo cha kusimamia amani
23 Desemba 2022Matangazo
Mwezi Novemba pande hizo hasimu zilitangaza kusitisha mapigano kwenye jimbo la kaskazini la Tigray, ambako maelfu ya watu wameuawa katika mapigano ya miaka miwili.
Miongoni mwa masharti ya makubaliano hayo ni kipengele cha kuanzisha chombo cha kufuatilia na kuzingatia ili pande zote mbili ziwe na uhakika kwamba mpango huo unafanikishwa.
Hilo lilikamilishwa jana na makamanda wa jeshi kutoka serikali ya Ethiopia na kundi la Wapiganaji wa Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF, katika mkutano uliofanyika kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Pembe ya Afrika, IGAD, Workneh Gebeyehu, amesema kuanzishwa kwa chombo cha pamoja ni "ushuhuda wa wazi" wa pande zote kuheshimu makubaliano ya amani.