Ethiopia na Eritrea
30 Novemba 2007Leo Nov.30,linamalizika jukumu iliopewa Tume ya mpaka kati ya-Ethiopia na Eritrea.Ikitazamiwa mahasimu hao 2 wenye ugomvi wa mpaka ,wataiwachia siku hii kupita -muda wa mwisho uliotolewa na UM kukubaliana mpaka wao.Kuamkia kesho tarehe mosi, Desemba, mpaka wa km 1000 unaobishaniwa na nchi hizi 2 tangu vita vyao vya 1998, utakua umechorwa upya.Lakini utabakia hivyo karatasini tu.
Kwa muujibu wa wachunguzi,mabishano ya maneno kati ya Addis Ababa na Asamara ya hivi karibuni, yaashiria vitavipya.
Kuepusha balaa jipya, tangu katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon hata serikali ya Marekani wamezitaka pande zote mbili kumtuliza shetani,haioneshi mwito wao unasikilizwa.
“Nilikwisha sema na narejea tena kusema:
Kamwe hatutanadi vita dhidi ya Eritrea,isipokua imeivamia Ethiopia.Hapa si kusudii uchokozi wa hapa na pale ,bali uvamizi hasa.Hiyo ndio itakayokua sababu pekee kwetu kupigana vita na Eritrea.Siamini lakini,kuwa Eritrea itafanya ujasiri kama huo,kwani yajua hapo itacheza na moto.
Naamini kwahivyo, kumalizika kwa muda wa jukumu la Tume ya mipaka kutapita kwa amani kama ilivyokua siku zote tangu kuanza karne mpya ya kiothodox nchini Ethiopia.”
Ali Abdu,waziri wa habari wa Eritrea,jibu lake kwa waziri mkuu Zenawi lilikua hili:
“Tume ya mipaka EEBC imeuarifu ulimwengu mzima kwamba Eritrea, imetimiza masharti yote iliopewa.Mpira sasa uko katika lango la Ethiopia.”
Sasa tangu maneno makali kati ya Addis Ababa na Asamara yamefikia kilele chake; na tangu Meles zenawi wa Ethiopia hata Afewerki wa Eritrea, wamebanwa sawa sawa katika siasa zao za ndani nchini,wachunguzi wanahisi ni swali la wakati tu lini vita vitaripuka tena.
Muandishi habari wa kingereza Michela Wrong,ametumika miaka mingi barani Afrika na ni muadishi wa kitabu alichokiita “Jinsi gani dunia ilivyoihini nchi ndogo ya kiafrika ya Eritrea”.
Amekumbusha , “Tume ya mipaka iliarifu kuwa jukumu iliopewa linamalizika mwishoni mwa mwezi huu na ikifika siku hii, haitakuwapo tena.Hapo tena mpaka utakua umeshachorwa na kuwekewa alama hata ikiwa haukusimamishiwa nguzo za seruji.Hofu ni kuwa, tarehe hii ya mwisho yaweza ikaripua wimbi jipya la mapigano kwa sababu Ethiopia hairidhiani kabisa na siasa ya tume ya EEBC na haikuruhusu kuwekwa alama mpaka unapopita.
Wakati wa kuanzisha vita ni muwafaka kwa jeshi la Ethiopia.Kwani, hivi sasa, wao ndio wanaozima moto nchini Somalia.Na kwavile, Addis Ababa ambayo inajigamba kuwa ndio ngome ya kikristu dhidi ya waislamu wenye itikadi kali katika pembe ya Afrika,ikijitosa kwa vita vyengine nchini Eritrea,haitaapizwa .