Ethiopia, Misri na Sudan kuanza tena mazungumzo kuhusu bwawa
26 Oktoba 2020Matangazo
Akizungumzia kerejea tena kwa mazungumzo hayo, rais wa Afrika Kusini ambaye pia ni mwenyektii wa Umoja wa Afrika, Cyril Ramaphosa amesema hatua hiyo ni ishara ya kuwepo imani kwenye mchakato huo wa mashauriano unaoongozwa na bara la Afrika.
Kuanza tena mazungumzo hayo kunakuja ikiwa ni siku mbili tangu Ethiopia ilipomwita balozi wa Marekani nchini humo kulalamika kuhusu matamshi ya rais wa Marekani yaliyotafsiri kuchochea vita kati ya Misri na Ethiopia.
Ijumaa iliyopita rais Donald Trump alitoa wito wa kufikiwa makubaliano kati ya mataifa yanayozozana na kuongeza mzozo huo umefikia pabaya na kwamba Misri inaweza kufikia uamuzi wa kulishambulia bwawa hilo la Ethiopia.