Ethiopia imerefusha kwa mwezi mmoja zaidi sheria inayopiga marufuku maandamano mjini Addis Ababa
14 Juni 2005Matangazo
Madhamana wa serikali ya Ethiopia wamerefusha kwa mwezi mmoja zaidi sheria inayopiga marufuku maandamano mjini Addis Ababa.Sheria ya awali iliyotangazwa kati kati ya mwezi uliopita, muda wake ulikua umalizike wiki hii.Wiki iliyopota watu 36 waliuwawa kufuatia machafuko katika mji mkuu wa Ethiopia,waandamanaji walipokua wakilalamika dhidi ya visa vya udanganyifu uchaguzi wa bunge ulipoitishwa may 15 iliyopita.Wakati huo huo muunganao wa upande wa upinzani umesema mbunge wao mmoja amepigwa risasi na kuuliwa na polisi mwishoni mwa wiki iliyopita.Shirika la haki za binaadam la Ethiopia linasema wapinzani elfu tatu wametiwa mbaroni kufuatia maandamano ya wiki iliyopita.