1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia, Egypt, Sudan zaanza mazungumzo ya Mto Nile

23 Septemba 2023

Ethiopia imesema leo hii imeanza duru ya pili ya mazungumzo na Misri na Sudan kuhusu bwawa lenye utata la kuzalisha nguvu ya umeme linalojengwa na Ethiopia.

https://p.dw.com/p/4WjEc
Äthiopien Renaissance-Staudamm
Picha: Minasse Wondimu Hailu/AA/picture alliance

Ethiopia imesema leo hii imeanza duru ya pili ya mazungumzo na Misri na Sudan kuhusu bwawa lenye utata la kuzalisha nguvu ya umeme linalojengwa na Ethiopia kwenye eneo la Mto Nile, ujenzi ambao umekuwa chanzo cha mvutano wa muda mrefu kati ya mataifa hayo matatu. Kupitia ukurasa wa X, zamani ukijulikana kama Twitter, wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imesema imejitolea "kupata suluhisho kwa mazungumzo ya kirafiki kupitia mchakato unaoendelea wa pande tatu."Mapema mwezi huu, Ethiopia ilitangaza kukamilika hatua ya nne ya na ya mwisho ya kazi ya ujazaji kwenye bwawa hilo linalojulikana kama  Grand Renaissance, na hivyo kuikasirisha na Misri ambayo ilishutumu hatua hiyo kuwa ni kinyume cha sheria.Misri na Sudan zinahofia bwawa hilo kubwa, ambalo ujenzi wake umegharimu dola bilioni 4.2, litapunguza kwa kiasi kikubwa sehemu ya maji ya Mto Nile wanayoyapata kwa matumizi yao ya kila siku na mara kadhaa wameiomba serikali ya Addis Ababa kusitisha kulijaza hadi yafikiwe makubaliano baina yao.