Eskinder Mamo na Amanuel Abrha kutoka Ethiopia walikutana kama wanafunzi nchini Ujerumani. Ndiko walikoanzia kutafuta njia za kutimiza ndoto zao: Kurudi Ethiopia na kujenga kampuni ya mawasiliano ya teknolojia. Miaka miwili iliyopita, walithubutu kuikabili changamoto hiyo kwa fedha walizokopa kutoka kwa ndugu. Na sasa kampuni yao ndogo ndiyo kwanza imezindua huduma maalumu katika soko la Ethiopia.