Eritrea yatuma maafisa wake Ethiopia
25 Juni 2018Shirika la habari la serikali ya Ethiopia hata hivyo halijatoa maelezo zaidi kuhusu ujumbe huo wa Eritrea.
Eritrea na Ethiopia wamekuwa maadui wakubwa tangu walipoanzisha mapigano ya mpakani kuanzia mwaka wa 1998 hadi 2000 ambayo yaliwauwa watu 80,000.
Uhasama uliendelea huku Ethiopia ikikataa kuondoka katika mpaka uliopewa Eritrea kama sehemu ya ugawaji wa mpaka mnamo mwaka wa 2002.
Lakini mwezi huu, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisema sasa atakubali ugawaji wa mpaka huo.
Eritrea, mkoa wa zamani wa Eathiopia, ilitangaza uhuru wake mwaka wa 1993 na kuifanya Ethiopia kuwa nchi isiyo na bandari.
Mkutano huo wa wajumbe wa Eritrea umepangwa licha ya mripuko wa Jumamosi katika mkutano wa hadhara wa serikali wakati Abiy alikuwa akitoa hotuba kwa maelfu ya wafuasi wake mjini Addis Ababa.