1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan awasili Berlin, Ujerumani kwa ziara fupi

17 Novemba 2023

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amewasili mjini Berlin, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini Ujerumani ndani ya miaka mitatu.

https://p.dw.com/p/4Z3fR
Erdogan amtembelea Scholz Ujerumani
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Uturuki Tayyip ErdoganPicha: INA FASSBENDER/AFP/Getty Images;Adem Altan/AFP/Getty Images

Kwenye ziara yake inayotarajiwa kuwa ya saa chache tu, Erdogan anakutana na rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na atafanya mazungumzo na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz baadaye kabla ya kurudi nchini mwake usiku wa leo.

Hata hivyo ziara ya Erdogan ina utata kutokana na kauli zake kuhusu Vita vya Israel dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Rais Erdogan kuizuru Ujerumani leo

Erdogan hulitaja Hamas kuwa “kundi la ukombozi" na hulaani oparesheni za kijeshi za Israel kama uhalifu wa kivita, akiishutumu Israel kwa kile alichokiita "ugaidi unaofanywa na serikali."

Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya zimeliorodhesha Hamas kama kundi la kigaidi. Ujerumani, kwa upande mwingine, husema usalama wa Israel ni “jukumu lake la kiserikali."