1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan ataratajia ukurasa mpya wa uhusiano na Ujerumani

Oumilkheir Hamidou
27 Septemba 2018

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anaanza ziara rasmi ya siku mbili nchini Ujerumani kuanzia leo (27.09.2018). Lengo la ziara hiyo ni kuweka kando mivutano ya miaka iliyopita iliyochafua uhusiano kati ya nchi mbili.

https://p.dw.com/p/35Z3u
Türkei Präsident Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip ErdoganPicha: picture-alliance/AA/M. Cetinmuhurdar

Uhusiano kati ya Berlin na Ankara umevurugika tangu miaka kadhaa iliyopita. Kwamba serikali ya Uturuki inawawekea vizuwizi wanasiasa wa Ujerumani wanaotaka kukitembelea kituo cha jeshi la wanaanga wa Ujerumani cha Incirlik, na kufuatiwa baadae na kukamatwa  raia wa wajerumani nchini Uturuki na tuhuma za Erdogan Ujerumani inafuata mitindo ya wanazi, ni mojawapo ya vyanzo vya mivutano. Kiini cha ugonvi ni mwelekeo wa kimabavu unaofuatwa na serikali ya Erdogan.

Hivi sasa lakini serikali ya Uturuki inajaribu kuijongelea upya Ujerumani na Ulaya. Viongozi mjini Ankara wanataraji viongozi wa mijini Berlin na Brussels watawasaidia kurejesha hali ya utulivu nchini mwao baada ya mivutano kuzidi makali kati ya Uturuki na Marekani kwasababu ya hitilafu za maoni kuhusiana na mzozo wa Syria, kutokana na kukamatwa adri wa kimarekani nchinin Uturuki na pia kufuatia vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Uturuki.

Pande zote zaazimia kumaliza mvutano na kusonga mbele

Tangu Berlin mpaka Ankara viongozi wamepania kuona uhusiano unarejea kuwa wa kawaida na ziara  ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan itakayoanza september 27 hadi 29 inaweza kuwa hatua ya mwanzo kulifikia lengo hilo.

Deutschland Demonstration gegen Erdogan in Berlin
Wapinzani wa ziara ya Erdogan wakiandamana mjini BerlinPicha: picture-alliance/dpa/P. Zinken

Serikali ya Ujerumani inajiwekea matumaini makubwa. Msemaji wa siasa ya nje wa vyama ndugu vya CDU/CSU Jürgen Hardt anataka Erdogan adhihirishe kwamba anathamini maadili ya ulaya,maadili ya uhuru wa mtu kutoa maoni yake na uhuru wa vyombo vya sheria.

Hatua za kujongeleana zitawezekana tu ikiwa raia wa Ujerumani wanaoshikiliwa jela nchini Uturuki, wataachiwa huru.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya ujerumani raia watano wa ujerumani wanashikiliwa kizuwizini nchini Uturuki.

Rais wa Uturuki atakaribishwa kwa hishma za kijeshi ijumaa asubuhi na rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier katika kasri la Bellevue. Ijumaaa usiku ataandaliwa karamu rasmi ya hishima katika kasri hilo-suala linalozusha mabishano makubwa humu nchini.

Ususiaji wa wanasiasa

Wanasiasa kadhaa wa ngazi ya juu wameshasema hawatohudhuria karamu hiyo. Miongoni mwao ni mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Free Democrat Christian Lindner, na mwenyekiti wa zamani wa chama cha walinzi wa mazingira Cem Özdemir . Kansela Merkel hatoshiriki pia katika karamu hiyo. Lakini hiyo si ajabu kwasababu kawaida kansela hahudhurii karamu kama hizo. Hata hivyo kansela Angela Merkel atakutana mara mbili na rais Erdogan atakapokuwa ziarani nchini Ujerumani.

Hali ya kiuchumi nchini Uturuki ndio mada inayotazamiwa kugubika mazungumzo.Hata kama rais werdogan anashikilia uchumi wa nchi yake ni imara vya kutosha kuweza kudumu kishindo kilichoko.Hata hivyo kudhoofika sarafu ya nchi hiyo, ughali wa maisha na idadi kubwa ya wasiokuwa na kazi ni mambo yanayoutikisa uchumi wa Uturuki.

Mwandishi: Serdar, Seda/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Khelef