1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan apongeza ujasiri wa ICC kwa viongozi wa Israel

23 Novemba 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan leo hii alisifu "uamuzi wa kijasiri" wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kutaka kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa ulinzi Yoav Gallant.

https://p.dw.com/p/4nLkP
Aserbaidschan | COP29 in Baku | Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa 29 wa viongozi wa dunia kuhusu hali ya hewa.Picha: DHA

Katika hotuba yake mjini Istanbul amesema wanadhani ni muhimu kwamba uamuzi huo wa kijasiri ufanywe na wanachama wote wa mkataba uliounda mahakama hiyo kwa kurejesha imani ya ubinadamu katika mfumo wa kimataifa. Mahakama ya ICC ilitoa waranti dhidi ya viongozi wa Israel na mkuu wa jeshi la Hamas Mohammed Deif siku ya Alhamisi kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita katika mzozo wa Gaza.