SiasaUturuki
Erdogan ameashiria ataunga mkono kuikaribisha Finland NATO
30 Januari 2023Matangazo
Katika hotuba aliyoitoa kwa ajili ya vijana wa Uturuki, Erdogan amesema nchi yake inaweza kuridhia Finland kuwa mwanachama wa NATO lakini siyo Sweden, anayoituhumu kuyaunga mkono makundi yaliyopigwa marufuku nchini Uturuki.
Soma pia:Uturuki yachukuwa hatua dhidi ya uchomaji Quran barani Ulaya
Ingawa serikali ya Erdogan inayalaumu mataifa yote mawili kwa kuwasaidia wapiganaji wa Kikurdi nchini Uturuki, msimamo wake kuelekea Sweden umetiwamakali na kitendo cha wiki iliyopita ambapo mwanasiasa wa mrengo mkali nchini Sweden aliichoma moto Quran Tukufu mbele ya ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm.
Kufuatia kitendo hicho Erdogan alisema Sweden haiwezi tena kuitegemea Uturuki kuisaidia kupata unachama wa NATO.