Elon Musk kushitakiwa Brazil
8 Aprili 2024Matangazo
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Musk anatuhumiwa kwa kuzuwia sheria kuchukuwa mkondo wake.
Mmiliki huyo wa mtandao wa X anapingana na uamuzi wa Jaji Moraes ulioutaka mtandao huo wa kijamii kuzifungia baadhi ya akaunti za watumiaji.
Soma zaidi: Twitter yaondowa alama ya buluu kwenye akaunti za watu mashuhuri
Mapema hapo jana, Musk alituma ujumbe kwenye mtandao huo akisema X itaondowa zuio dhidi ya watumiaji hao kwa kuwa ni kinyume na katiba.