Eliud Kipchoge ashinda tuzo ya Asturias
18 Mei 2023Matangazo
Shirika la Uhispania linalosimamia tuzo hiyo, limetangaza hayo leo.
Kipchoge mwenye umri wa miaka 38 ambaye ameshinda medali za dhahabu katika mbio za masafa marefu za mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 na 2020, anachukuliwa kuwa mwanariadha bora ulimwenguni wa mbio za masafa marefu.
Aliwahi pia kushinda mbio za mita elfu 5,000 katika mashindano ya ulimwengu mwaka 2003.
Shirika hilo limesema Kipchoge ambaye pia ameshinda mashindano ya Berlin na London marathion mara nne, anafahamika kama mwanafalsafa kutokana na juhudi na mikakati yake kwenye mashindano.
Tuzo hiyo yenye thamani ya euro 50,000, ni kati ya tuzo nane ambazo hukabidhiwa waliofanya vyema katika Nyanja za Sanaa, mawasiliano, sayansi na fasihi.