Kipchoge bingwa tena
29 Aprili 2019Matangazo
Kipchoge ndiye anayeshikilia rekodi ya kasi zaidi katika marathon baada ya kuandikisha muda wa kasi zaidi duniani alipokimbia kwa 2:01:39 katika marathon ya Berlin, Ujerumani mwaka jana.
Mkenya huyo amekimbia jumla ya marathon 12 na kushinda 11.
Muingereza Sir Mo Farah ambaye wengi walitazamia ampe ushindani mkubwa Kipchoge, hakufua dafu na akamaliza katika nafasi ya tano.
Upande wa wanawake bingwa mtetezi Vivian Cheruiyot kutoka Kenya aliishia kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Bridget Kosgei.