1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Elimu Kwa Wote: Wasomi wanapoondoka

25 Juni 2012

Watu wenye akili hupata nafasi za kazi kwa urahisi. Iwapo hakuna ajira nchini kwao, basi wanaweza kuhama. Hivi sasa yapo mawazo yanayotaka kuzisaidia nchi masikini ili zisiathirike na uhamiaji wa wasomi.

https://p.dw.com/p/15Ie2
health; medicine; doctor; healthcare; medicalcare; surgeon; stethoscope; hospital; portrait; x-ray; radiography; radiograph; checking; examining; man; black; african; African-American; male; cheerful; joyful; ethnicity; culture; diversity; 30 years old; looking at camera; office; working; student; indoors; health; medicine; doctor; healthcare; medicalcare; surgeon; stethoscope; hospital; portrait; x-ray; radiography; radiograph; checking; examining; man; black; african; african-american; male; cheerful; joyful; ethnicity; culture; diversity; 30 years old; looking at camera; office; working; student; indoors goodluz - Fotolia.com
Picha: Fotolia/goodluz

Tatizo la kuhama kwa wasomi vijana linazikumba nchi nyingi zinazoendelea. Benki kuu ya dunia inakadiria kwamba bara la Afrika linapoteza wasomi wapatao 23,000 kila mwaka. Watafiti kutoka Canada wamepiga hesabu na kutabiri kwamba nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara hupoteza kiasi cha dollar billioni mbili za Kimarekani kila mwaka kwa sababu ya madaktari waliosomea katika nchi hizo na kisha kuhamia katika nchi nyingine kwa ajili ya kufanya kazi. Ukweli ni kwamba mahesabu haya ni ya kweli kwa sehemu tu. Wahamiaji hutuma kiasi fulani cha mishahara yao kwa familia na marafiki nyumbani. Kiasi hiki cha fedha ni kikubwa sana na ni mara mbili ya kiasi cha fedha za misaada kinachotolewa na nchi zilizoendelea.

Uhamiaji wa mzunguko unawezekanaje?

Mbali na hayo, baadhi ya wataalamu hao wenye ujuzi wa hali ya juu, hurejea katika nchi zao baada ya miaka kadhaa ya kuishi ugenini wakiwa na lengo la kufanya kazi huko au hata kuwekeza fedha walizozipata wakiwa wanafanya kazi nje ya nchi. Jambo hili linafahamika kama "uhamiaji wa mzunguko". Huu ndio mkakati unaofuatwa katika kupambana na uhamiaji wa wasomi.

Mmoja wa watu wanaounda mikakati ya aina hiyo ni Stefan Angenendt kutoka wakfu wa Taaluma na Siasa wa hapa Ujerumani. Kwa miaka kadhaa sasa, mtaalamu huyo amekuwa akifuatilia wahamiaji wanaokuja kuishi Ujerumani. Angenendt amegundua kuwa ni wahamiaji wachache tu wanaoondoka makwao na kuamua kuishi ugenini moja kwa moja. Vijana wengi hurudi katika nchi wanazotokea baada ya muda fulani au huamua kusafiri kutoka Ujerumani na kwenda nchini kwao mara kwa mara. "Hii ni kwa sababu sasa kuna njia nyingi za usafiri," anaeleza Angenendt. "Zipo njia za usafiri za gharama nafuu. Watu wamejenga mitandao ambayo inawarahisishia kuondoka makwao na kuhamia nchi nyingine kwani tayari wanakuwa wanafahamu baadhi ya watu katika nchi wanayotaka kuhamia."

Hata hivyo sheria zinazowaruhusu wahamiaji wenye ujuzi mkubwa kuingia Ujerumani bado  ni kali sana. Kwa sababu hiyo, Angenendt anataka pawepo na utaratibu utakaowawezesha wahamiaji kuamua wakati ambapo watapenda kurudi makwao. Vile vile wahamiaji wanatakiwa kupewa msaada na pia kupewa ushauri pindi wanapoamua kurudi katika nchi zao na kuanza maisha yao huko.

Faida mara tatu

Gunilla Finke, ambaye ni mkurugenzi wa kamati inayosimamia wakfu zinazoshughulika na utengamano na uhamiaji anasema kuwa uhamiaji wa mzunguko unaleta faida mara tatu. Mambo yote yakienda ipasavyo, mhamiaji atafaidika kwa sababu anapata mshahara mkubwa zaidi Ujerumani kuliko katika nchi anayotoka na kwa sababu anaweza kupata ujuzi zaidi, Ujerumani inafaidika kwa sababu mhamiaji anakuja na ujuzi unaohitajika nchini hapa na hata nchi anayotokea mhamiaji inapata faida kwani mhamiajai anaporudi nyumbani analeta ujuzi na tajiriba zaidi. Lakini haya yote yanaambatana na tatizo moja: hakuna mtu anayefahamu namna ya kuleta faida hizi moja kwa moja.

Dr. Gunilla Fincke vom Sachverständigenrat deutscher Stiftungen für Integration und Migration (SVR). Copyright: David Ausserhofer 2012
Wataalamu wa uhamiaji kama Dr. Gunilla Fincke anahitaji msaada zaidi kwa uhamiaji wa mzungukoPicha: David Ausserhofer

Mawazo mengi pasipokuwa na mkakati maalum

Badala yake zipo programu nyingi zinazofuata mbinu tofauti tofauti. Tofauti ya programu hizo zinaanzia katika misaada kwa ajili ya elimu: baadhi ya nchi hutoa mikopo yenye riba ya chini kwa ajili ya masomo katika nchi za Ulaya au Marekani. Mikopo hiyo inaambatana na masharti kwamba atakayesomeshwa na lazima arejee katika nchi anayotoka baada ya kumaliza masomo yake. Mawazo mengine yanayolenga kuleta faida za uhamiaji ni misaada ya masomo inayotolewa na Umoja wa Ulaya ambayo inalenga kuwezesha uhamiaji wa wanafunzi na wataalamu kutoka nyanja mbali mbali. Lakini licha ya hayo suala la uhamiaji wa mzunguko si rahisi sana. Hii ni kwa sababu wapo watu wenye kutafuta maslahi yao binafsi.

Wanafunzi kutoka nje katika chuo kikuu Ujerumani
Wanafunzi wanaosoma nje wanaweza kuungana na mitandao muhimuPicha: picture alliance/dpa

Wanasiasa wengi wa Ujerumani hawako tayari kuondoa vikwazo vinavyowazuia watu kuhamia nchini kwao kwa sababu wanaogopa kuwakasirisha wapiga kura. Wanafahamu fika kuwa pindi watakapowaruhusu wahamiaji wengi zaidi kuingia nchini, raia wengi wa Ujerumani watahofia kupoteza nafasi zao za kazi. Kwa upande mwingine, mashirika ya kibiashara yanataka wahamiaji wengi zaidi waruhusiwe kuingia Ujerumani kwani mashirika hayo yanahitaji wafanyakazi wenye ujuzi wa hali ya juu wanaotokea katika nchi za nje. Hata hivyo makampuni hayo yanataka kuwaajiri wahamiaji hao kwa muda mrefu na si kwa kipindi kifupi tu.

Mwandishi: Klaus Dahmann

Tafsiri: Elizabeth Shoo

Mhariri: Mohammed Khelef