1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eintracht Frankfurt

Ramadhan Ali5 Juni 2007

Eintracht Frankfurt ilitwaa ubingwa wa Ujerumani 1959 na kombe la shirikisho (DFB) mara 4.

https://p.dw.com/p/CHc2

Mashabiki wa Afrika,wanaikumbuka Eintracht Frankfurt- kuwa timu walioichezea mastadi wa 2 wa dimba wa Afrika-Mghana- Anthony Yeboah na Mnigeria-J.J.Okocha.Mara 2 Yeboha aliibuka mtiaji mabao mengi katika Bundesliga hapo 1993-94 akiichezea Frankfurt .Okocha akizikosha nyoyo za mashabiki na sio tu wa Frankfurt bali wa Bundesliga nzima kwa chenga zake za ajabu na pasi zake maridadi.

Eintracht Frankfurt ni mojawapo wa timu zilizoanzisha bundesliga hapo 1963 na ingawa hawakutawazwa tangu wakati huo mabingwa, walikaribia mno msimu wa 1993 walipocheza na mzinga wao Anthony yeboha na mchawi wao wa chenga J.j.Okocha.Hatahivyo, Frankfurt imetwaa mara 4 kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani-DFB pokale.Ilitawazwa pia mabingwa wa Ujerumani mara 1,lakini hii ilikuwa 1959 kabla kuanzishwa kwa Ligi ya sasa –Bundesliga.

Frasnkfurt inakumbwa pia kwa wachezaji 2 maarufu sana –Jürgen Grabowski na Bernd Hölzenbein-waliokua ufunguo wa ushindi wa kombe la dunia 1974 nchini Ujerumani.

Kama FC cologne, Eintracht Frankfurt nayo imeonja miaka ya karibuni shubiri ya kuteremshwa daraja ya pili na baadae kupanda ya kwanza.Na baada ya kucheza finali ya Kombe la Shirikisho la kabumbu la Ujerumani mwaka 2006,msimu wa mwaka huu Frankfurt ilitia for a hadi nusu-finali na kwa kuzishinda timu kama Munich na Bremen ilimudu Frankfurt kuzuwia msimu huu kurudi daraja ya pili ambako inadai haistahiki kucheza.

Wimbo huu ni maarufu katika masikio ya mashabiki wa Frankfurt:

“Tumeiona Eintracht Frankfurt ikicheza katika finali.Ikicheza uzuri kabisa na staid wake Jürgen Grabowski.”

Grabowski asema:

“Hatukuteremshwa daraja ya pili.Lakini hiyo haiwezi kubakia shabaha yetu kuwa hatuteremshwi chini.Inatupasa kuwa na shabaha kubwa zaidi bila kufumbia macho upinzani mkali uliopo kwenye Bundesliga.Frankfurt imekuwa na dosari hivi karibuni la kushindwa kuwika nyumbani tena mbele ya mashabiki wa kima cha wastani cha 46.000 kwa kila mchezo uwanja mwake.”

Jürgen Grabowski ambae alibakia mtiifu kwa timu yake kwa muda wa miaka 15 na aliichezea mechi hadi 400 bila kubidi kubadilishwa,ndio ufunguo wa mafanikio ya klabu hii ya Frankfurt iliposhinda kombe la Ujerumani 1974 na 1975.

“Mabao 3:1 Frankfurt imeikomea Hamburg na kwa ushindi huo kwa mara ya kwanza katika historia yake imetwaa kombe la Ujerumani.”

Alisimulia mtangazaji uwanjani:

Miaka iliofuatia hapo,Frankfurt haikuwa ikigonga vicha vya habari vya kupendeza:Ilijionea kupungua heba kwa wachezaji wake na mara kwa mara ikibadili makocha wake –miongoni mwao felix Magath na Jupp Heynckey.Pia kinyan’ganyiro cha madaraka katika uongozi wake kimeongoza pia kuporomoka kwa klabu hii mnamo miaka ya kwanza ya 1990.Badala ya kutamba kwa Eintracht Frankfurt ilianza kuporomoka chini:1996 baada ya kuachwamkono na Yeboha na Okocha, Frankfurt iliteremshwa daraja ya pili ya Bundesliga.

Chini ya kocha wake wa sasa Friedhelm Funkel,Frankfurt imeanza kujiimarisha tena na kuna kila ishara kwamba Eintracht Frankfurt maskani mwake ni daraja ya kwanza ya Bundesliga.