1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECOWAS yaweka majeshi tayari kumvamia Jammeh

23 Desemba 2016

Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, inasema imeweka kikosi cha wanajeshi kwenye hali ya tahadhari, tayari kuingia Gambia endapo Rais Yahya Jammeh wa Gambia hataondoka madarakani.

https://p.dw.com/p/2Un69
Gambia Wahlen Yahya Jammeh
Picha: Getty Images/AFP/M. Longari

Akizungumza kupitia televisheni ya taifa ya Mali, rais wa jumuiya hiyo, Marcel de Souza, amesema viongozi wa ECOWAS wanampa muda Jammeh kuondoka kwa heshima, lakini kama hataki kuitumia fursa hiyo, basi wanajeshi watatumwa kumuondoa ifikapo tarehe 19 Januari, siku ya mwisho ya kumalizika kwa muhula wake madarakani. 

Jammeh ameapa kwamba atabakia madarakani, licha ya kushindwa kwenye uchaguzi wa tarehe 1 Disemba na mpinzani wake, Adama Barrow.

Mapema, ECOWAS ilikuwa imemuonya kwamba ingelichukuwa hatua zozote za lazima kuukwamuwa mkwamo wa kisiasa uliopo.