DW yatimiza miaka 65 tangu kuundwa
4 Juni 2018"Wapenzi wasikilizaji katika nchi za mbali ...." Ni maneno kutoka kwa kiongozi wa nchi. Kwa salamu hizo kutoka kwa rais wa Ujerumani Theodor Heuss DW ilianza rasmi tarehe 3,Mei mwaka 1953 kurusha matangazo yake. Ilikuwa dhahiri kwamba mwanzoni mwa matangazo hayo , "msikilizaji katika nchi za nje aliweza kupata taswira ya kisiasa , kiuchumi na kiutamaduni ya Ujerumani." Kwa matangazo ya mawimbi ya masafa mafupi DW kutoka Kolon ilifanikiwa katika lengo lake na kuwafikia pekee katika lugha ya Kijerumani wasikilizaji katika maeneo mengi ya dunia.
Mwaka 1954 ndipo yalianza matangazo ya baadhi ya lugha za kigeni. Mwaka 1992 matangazo ya televisheni yakaanza, na mara baada ya hapo DW ikaanza kusambaza habari pia kwa njia ya mtandao. Deutsche Welle imebadilika," baada ya miaka 65 amesema mkurugenzi Peter Limbourg. "Kutoka kuwa kituo cha utangazaji kinachorusha matangazo yake kwa masafa mafupi nje ya nchi na kuwa shirika la kimataifa la habari, ambapo lugha 30 zinarusha hewani matangazo yake, ambapo tunajaribu kwa kila linalowezekana kuwafikia watu kwa kila hali, kuwapatia taarifa ambazo katika nchi zao huchujwa kwanza ama kuzuiwa kabisa. Ni mabadiliko makubwa katika miaka hii 65." Bila shaka ilikuwa rahisi katika enzi zile za kurusha matangazo kwa masafa mafupi kuwafikia wasilikizaji katika kila kona ya dunia. "Lakini iwapo tusingebadilika, sijui tungekuwa wapi."
Leo hii kwa mujibu wa mkurugenzi wa DW utendaji wa hayo yote ni mgumu. Kwa hivi sasa kuna fursa nyingi za kuwafikia wasikilizaji wengi zaidi kuliko hapo awali kwa kupitia mtandao wa internet, mitandao ya kijamii na mfumo wa kuwa na redio washirika. Mkurugenzi anasema matangazo ambayo ni mchanganyiko wa taarifa ya habari, uchambuzi na msingi wa habari yenyewe, utangazaji wa kisasa ambao unawagusa wasikilizaji wa rika mbali mbali, na mara nyingi zikilenga katika kundi la vijana zaidi. Limbourg amekuwa kiongozi wa shirika hilo la DW kwa muda wa miaka karibu minne na nusu sasa na anataka kuimarisha umuhimu wa matangazo ya kimataifa.
Sherehe bungeni
Jumanne hii kutakuwa na sherehe maalum katika bunge la Ujerumani Bundestag za miaka 65 tangu kuanzishwa kwa matangazo ya shirika hilo la utangazaji. Watakaohudhuria ni pamoja na waziri wa utamaduni Monika Gruettes pamoja na wabunge kadhaa wa makundi yote ya vyama. Hususan mgeni rasmi atakuwa kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye atalihutubia bunge. Na kansela anajifahamisha kuhusiana na mradi wa hivi sasa wa matangazo, ambao ni kuhusu uelekezi wa vidio katika lugha ya Kirusi , ambao utasaidia , kuzuwia habari za uongo.
Tafsiri hali ya "matangazo haya" ni pana: Matangazo ya televisheni katika lugha nne, taarifa katika mtandao wa internet kwa lugha 30 pamoja na shughuli mbali mbali katika mitandao ya kijamii. Simu za mkononi za kisasa zina umuhimu mkubwa katika kupashana habari. Msikilizaji wa kweli katika enzi hizi kwa kiasi kikubwa ni kijana.
Kile ambacho Wajerumani hawakijui ni kwamba Kituo cha mafunzo cha DW , zamani shirika la kimataifa la maendeleo ya vyombo vya habari . limefanikiwa kuwafunza maelfu ya waandishi habari tangu mwaka 1965. Kwa hiyo mawaziri wa Ujerumani hukutana na watu wenye uwezo mkubwa nje ya nchi kwa ajili ya mazungumzo, ambao wamepata mafunzo katika chuo hiki cha DW.
Baadhi ya masuala mengine magumu ya kisiasa duniani yanafanana na wakati wa kuundwa kwa DW miaka 65 iliyopita. Baadhi ni pamoja na matamshi ya wakati wa enzi za vita baridi, kutoa mawazo pamoja na uhuru wa vyombo vya habari umo hatarini. Wakati umekuwa mgumu sana , ikiwa na maana kazi nyingi zaidi kwa DW.
Changamoto za enzi hizi
Tunapaswa kutoa taarifa, kujenga madaraja na kusambaza maadili, " amesema mkurugenzi mkuu wa DW Limbourg. Iwapo tutaiita enzi ya sasa ya vita baridi ama utaratibu wa mtengano duniani, changamoto kupitia propaganda , tarifa za uongo, uhamiaji, mabadiliko ya tabia nchi na ugaidi vinaongezeka.
Limbourg anazungumzia pia kuzuiwa kwa kiasi fulani kwa matangazo ya DW nchini China ama Iran. "Hali hii inatutia wasi wasi , lakini hali hii inaonesha pia, kwamba kazi yetu ina athari chanya." Leo hii kuna mapambano ya kimifumo na kinadharia pamoja na mbio za mashindano ya matangazo kimataifa.
"wafanyakazi ndio ufunguo wa mafanikio ya Deutsche Welle", imeelezwa katika misingi ya DW. Katika miji yote ambayo DW iko Bonn na Berlin kuna wafanyakazi wapatao 3400 kutoka mataifa zaidi ya 60 wanaofanyakazi. Kwa hiyo DW inamchanganyiko ya tamduni nyingi kuliko taasisi yoyote nchini Ujerumani. Idadi ya waandishi walioko nje ya Ujerumani katika bara la Afrika, Asia na Amerika kusini inaongezeka. "Mchanganyiko huu wa tamaduni ni hazina kubwa katika uwezo wa matangazo yetu, anasema mkurugenzi mkuu Limbourg.
Mwandishi: Christoph Strack / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Iddi Ssessanga