DURU YA PILI YA KOMBE LA AFRIKA YAANZA JUMAMOSI KWA TUNISIA...
5 Februari 2004Duru ya pili ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Tunisia, inaanza alaasiri ya jumamosi kwa timu mbili za Afrika ya magharibi-Mali na Guinea kuingia uwanjani.
Baadae wenyeji Tunisia wataingia uwanjani katika mpambano wapili na makamo-bingwa wa Afrika -simba wa Senegal.Tunisia kama wenyeji wa mashindano haya walikuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya duru hii ya robo-finali lakini sherehe zao za ushindi dhidi ya Kongo ziligubikwa na vilio vya udanganyifu.Hatahivyo, tunisia ilikata tiketi yake kwa changamoto ya jioni hii na senegal kwa kuizaba Kongo mabao 3-0.Dharuba ilizuka pale nahodha wa Kongo Lomana LuaLua alipotolewa nje ya uwanja katika kipindi cha kwanza na rifu na hii iliwapa nafasi wenyeji kuteremka mlima hadi robo-finali ya jioni hii.
Guinea iliibuka nafasi ya pili katika kundi hili ikichukua pointi 4 kwa 6 za tunisia.Rwanda ilifuata nafasi ya tatu.
Jumapili itakua asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano Monastir:huko simba wa nyika Kamerun wana miadi na super eagles Nigeria na wanaahidi kuwala ndege hao wahayi. Kamerun inatapia taji lake la 3 mfululizo katika Kombe hili na Nigeria lakini ndio waliotoroka na Kombe liliöpoaniwa mara ya mwisho miaka 10 nyuma mjini Tunis.Kamerun inadai mla ni mla leo, mla jana kala nini.
Dakika tu baada ya Nigeria kuitimua Benin kwa mabao 2:1 na kutia mfukoni tiketi yake ya mpambano wa kesho na Kamerun, iliamua kuimarisha timu.K ocha Christian Chukwu alifuta adhabu aliowapa mastadi 3 kwa kuvunja amri ya kutoka nje usiku-Viktor Agali wa klabu ya Bundesliga ya Schalke,Celestian Bayayero wa Chelsea na mshambulizi wa Portsmouth ya Uingereza Yakubu Aiyegbeni.Wote waweza wakitaka kurejea waliambiwa.
Tukisubiri basi msisimko wa kesho kati ya simba wa nyika-Kamerun na Super Eagles Nigeria,hebu tuikague duru ya kwanza ya kombe hili jinsi ilivyokwenda na imeonesha maendeleo gani kwa dimba la Afrika:
Uklija upande wa matarajio,msisimko,mabishano na magoli,kombe la 24 la Afrika limetimiza yote hayo.Mabao mengi kupita mashindano ya hapo kabla .Kuna wachezaji waliotimuliwa kambini na kurudishwa nyumbani na halafu wakaitwa tena kurudi.Kuna wale waliozipa mgongo klabu zao za Ulaya kuzichezea timu zao za taifa licha ya upinzani mkali na wale waliokua na uraia wa nchi mbili na kuamua ule wa asili yao kama Mali na Algeria.
Sasa duru ya kwanza imepita ile ya kutoana imeanza na duru hii kuanzia jioni hii inaahidi msisimko mkubwa:je, senegal imefaulu kumchezesha tena Roger Lemere,aliekua kocha wa tuimu ya Taifa ya Ufaransa katika Kombe lililopita la dunia kindumbwe-ndumbwe kingine na kuitoa timu yake ya Tunisia nje ya Kombe la Afrika la mataifa.Na watunisia watamfa ninini ingelitokea hivyo ?
Wenyerji tunisia wameimarishwa na stadi wao mzaliwa Brazil Santos.
Kamerun ambayo hasikutamba kama ilivyotam,ba katika Kombe la mashirikisho huko Ufaransa mwaka jana ilipoitoa Columbia na Brazil na kushindwa finali na Ufaransa, imenguruma hadi sasa hatahivyo kwa mabao ya Patrick Mboma alietia hadi sasa mabao 4 licha ya kwamba nusra aachwe nje ya timu hii.Kwa mabao hayo,Mboma ameshawanyamazishwa vinywa wakosoaji wake na ni mizinga yake ambayo kesho simba wa nyika itaitegemea kubomoa lango la wanigeria.
Wachezaji 3 wa kamerun Mboma,geremi na kipa Carlos Kameni wameibiwa saa zao za dhahabu chapa Rolex hotelini pamoja na vitita vikubwa vya fedha-hii inafuatia wizi.
Upande wa magoli,Kombe la 24 la Afrika hadi sasa limejaza mabao 65 hadi kabla changamoto za leo ukilinganisha na jumla ya mabao 48 katika kombe zima lililopita.Na hii ni rekodi mpya inayooonesha jinsi Kombe hili lilivyogeuka la kuhujumu-attacking football.
Timu 3 za Afrika yakaskazini -Tunisia,Morocco na Algeria, zimedhihirisha si za kuchezea na zilizozusha msangao kwa mchezo wao.Morocco imeshinda kundi D bila ya kulazwa hata mchezo mmoja.Algeria iliomaliza wapili nyuma ya kamerun katika kundi C,imegundua lulu katika safu ya wachezaji wake:Hocine Achiou aliupiga msumari wa kwanza na wapili katika jeneza la Mafirauni wa Misri katika kombe hili la afrika:kwanza alitoka na dimba mita 60 kati ya uwanja akaenda nao na kuwachenga walinzi wa Misri na kutia bao maridadi lililoipatia Algeria ya wachezaji 10 ushindi .Hii ilituklumbusha alivyofanya maradona katika Kombe la dunia huko mexico 1986.
Baadae akatia bao jengine lililoitoa Misri kabisa nje ya Kombe hili.
Kuna timu chipukizi ambazo zilikataa kutimiza hatima zilizoandikiwa kabla mpira kuanza:yaani kuaibishwa na kurejeshwa nyumbani mikono mitupu hata bila ya pointi:Rwanda,Zimbabwe na hata Kenya zilicheza bora zaidi kuliko mashabiki wao walivyotazamia bora zaidi kuliko maadui zao walivyowabashiria.
Zimbabwe ilimaliza kampeni yao katika Kombe la Afrika walikocheza kwa mara ya kwanza kama rwanda kwa ushindi wa mabao 2:1 dghidi ya Algeria ilioitoa Misri.Kenya ilivunja mwiko wa miaka 32 wa kutoshinda hata mechi moja katika Kombe la Afrika kwa kutoroka na pointi 3 kwa kuizaba Burkina faso mabao 3:0, tena mabao maridadi ajabu.Na Rwanda baada ya kuwatoa jasho wenyeji Tunisia,na kutia bao maridadi,walikuja kuilaza jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kutwaa ushindi wao wa kwanza katika Kombe la afrika kabla kurudi maziwa makuu.Rwanda imerudi nyumbani ikiaaminiimejifunza mengi kutoka Kombe hili la afrika na kuwatia shime majirani zao Burundi kuacha mzozo na kushughulikia zaidi kucheza dimba kama ilivyofanya rwanda baada ya mauaji ya 1994.Kwani dimba linaponesha pia madonda na kupooza nyoyo .
Bundesliga-Ligi ya Ujerumani ikirudi uwanjani jioni hii,mabingwa Bayern Munich walikwishavuliwa taji la Kombe la Taifa ambalo walitaka kulitwaa tena mwaka huu kuchanganya na lile la Ligi.Klabu ya daraja ya pili Alemannia Aaachen iliipiga kumbo Bayern Munich hapo jumatano kwa mabao 2:1 na kukata wao tiketi ya nusu finali kati yao na Borussia Mönchengladbach.
Viongozi wa Ligi Werder bremen wao walivuka chupuchupu walipotwaa mwishoe ushindi wa mabao 3-2 kutoka kwa Greuther Fuerth.B.Mönchengladbach iliilaza Duisburg kupitia mikwaju ya penalty.Bremen itacheza sasa na Luebeck.
Kwahivyo, nusu-finali ya kombe la taifa la Ujerumani msimu huu itaingiza timu 2 za daraja ya kwanza na 2 za daraja ya pili.Itakua maajabu ikiwa finali itazikumbanisha timu 2 za daraja ya pili huko Berlin.
Katika medani ya riadha -mashindano ya ukumbini-indoors- Berhane Adere wa Ethiopia alishindwa katika jaribio lake la kuvunja rekodi ya dunia katika masafa ya mita 3000 wanawake mjini Dortmund.Siku 4 kabla muethiopia huyo alivunja rekodi ya dunia ya masafa ya mita 5000 katika mashindano mengine mjini Stuttgart.Adere alimaliza mbio huko Doprtmund kwa muda wa dakika 8,33.05 sek.
Muafrika Kusini Hezekiel Sepeng alikuja wapili katika changamoto ya mita 800 nyuma ya Mrusi Yuriy Borzakovsky.
Katika ringi ya mabondia ,mbabe wa wezani wa juu ulimwenguni wa taji la WBC Lennox Lewis wa uingereza alitangaza anastaafu.Lewis alipewa muda na shirikisho la mabondia la WBC hadi Machi mosi kuamua kurudi ringini kutetea taji lake na Klitchko au kuliachia taji hilo.Mpambano wao uliopita ulimpatia ushindi wa chupuchupu.