1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUESSELDORF : Kesi ya Deutsche Bank yatupiliwa mbali

29 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoL

Mahkama ya Ujerumani imetupilia mbali taratibu za kisheria dhidi ya Kiongozi Mkuu Mtendaji wa Deutsche Bank Josef Ackerman na watu wengine watano kuhusiana na mzozo wa kuuzwa kwa kampuni ya Mannesmann hapo mwaka 2000.

Uamuzi huo ulitolewa leo hii unamaliza sakata la kisheria la muda mrefu ambalo liligubika mustkabali wa benki hiyo mashuhuri kabisa nchini Ujerumani.

Mahkama hiyo ya mkoa huko Duesseldorf imeidhinisha pendekezo la waendesha mashtaka ambalo linataka washtakiwa walipe jumla ya euro milioni 5.8 ili mashtaka dhidi yao yafutwe. Waendesha mashtaka wamesema malipo hayo sio faini na kwamba ile dhana ya kutokuwa na hatia inaendelea kubakia pale pale.

Watu hao sita walifikishwa mahkamani kwa mara ya pili mwishoni mwa mwezi wa Oktoba kutokana na bahshihi zilizozusha ubishi kwa wakuu wa kampuni ya simu ya Ujerumani Mannesmann wakati iliponunuliwa na kampuni ya Vodafone.