1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI : Waislamu watakiwa kuungana dhidi ya ugaidi

24 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CErA

Waislamu duniani wametakiwa kuungana dhidi ya ugaidi kufuatia mashambulizi ya Sharm el Sheikh nchini Misri ambayo yamealaaniwa karibu na vyombo vyote vya habari vya Kiarabu kuwa ni mashambulizi ya kishenzi ambayo hayotasaidia kitu kufanikisha mapambano yao.

Wengi ya waliouwawa katika mashambulizi hayo walikuwa ni Wamasri.

Rais Mohammed Khatami wa Iran ametowa wito wa kuchukuliwa kwa hatua ya kimataifa kupambana na aina zote za ugaidi na kueleza kwamba mashambulizi hayo yanakwenda kinyume na maadili na mafundisho ya Kiislam.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Hamid Reza Asefi amesema hapo jana mashambulizi hayo mapya yanaonyesha upumbavu wa Marekani katika msimamo wake wa kushughulikia wanamgambo wa Kiislam.Ametaka Marekani ibadili sera yake katika vita dhidi ya ugaidi na kuachana na undumila kuwili kwa kutowa ushirikiano wake kwa jumuiya ya kimataifa.