1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dubai: Kiongozi wa Waislamu aitisha amani Algeria

13 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEE3
Kiongozi wa wafuasi itikadi kali ya Kiislamu nchini Algeria, ambaye aliachwa huru hivi karibuni, alisema hiyo jana kwamba utumiaji wa nguvu ungesita tu iwapo mamlaka itawafungua wafungwa wote, kugunduliwa wale waliopotea na kusitishwa hali ya hatari nchini humo. Abassi Madani, mkuu wa chama kilichopiga marufuku, Islamic Salvation Front (FAS), aliiambia televisheni ya Kiarabu Al Jazeera, kwamba masharti hayo ni sehemu ya juhudi zilizosambazwa kwa viongozi wa wanajeshi na serikali pamoja na vyama vinginevyo, juu ya kukomesha utumiaji nguvu ambao umeikumba nchi hiyo ya Afrika Kaskazini zaidi ya mwongo mzima. Kiongozi huyo wa Kiislamu, ambaye sasa ana umri wa miaka 70, alikamatwa muda mfupi kabla ya serikali inayoungwa mkono na jeshi, kufuta matokeo ya uchaguzi wa bunge, ambayo yaliashiria ushindi wa chama cha FIS mwaka 1992, tukio ambalo lilichochea utumiaji wa nguvu karibu mwongo mzima, ambamo kadiri ya watu laki moja hadi laki moja na nusu waliuawa.