DR.RICE NCHINI JAPAN
18 Machi 2005Matangazo
TOKYO:
Waziri wa nje wa Marekani Dr.C.Rice amewasili Japan leo kuanzisha juhudi za Marekani za kuanzisha mazungumzo mapya na Korea ya kaskazini juu ya mradi wake wa kinuklia.Ana azma ya kuwatumia washirika wa Marekani barani Asia kuishinikiza Korea kaskazini kurudi katika meza ya mazungumzo.
Baada ya mazungumzo yake mjini Tokyo na waziri mkuu Koizumi,Dr.C.Rice anaelekea Korea ya Kusini.
Korea ya kaskazini imeitaka Marekani itake radhi kwa kuitaja Korea miongoni mwa tawala za kidikteta pamoja na Cuba,Iran,Syria na Zimbabwe.