1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa yaandaliwa

15 Aprili 2016

Huenda tukaona marudio ya fainali ya ligi ya Klabu Bingwa barani Ulaya katin ya Real Madrid na Atletico Madrid baada ya droo ya michuano ya nusu fainali kuandaliwa

https://p.dw.com/p/1IWcA
Fußball Atletico de madrid - FC Barcelona Pep Guardiola und Diego Simeone
Picha: picture-alliance/dpa/J. C. Hidalgo

Real ambao waliushinda mchuano huo 4-1 baada ya muda wa ziada, watashuka dimbani na Manchester City huku mkondo wa kwanza ukiwa kaskazini magharibi ya England.

Atletico, ambao waliwanyamazisha Barcelona katika robo fainali, watawaalika Bayern Munich katika mpambano wa mkondo wa kwanza. Hii ina maana kuwa kocha wa Bayern Pep Guardiola ameepuka kile kingekuwa ni nusu fainali ngumu kwake dhidi ya Manchester City, timu ya Premier Lweague ambayo atachukua usukani msimu ujao. Lakini ina maana pia kuwa huenda akakutana nayo katika fainali.

Infografik Champions League Auslosung Halbfinale 2015-16 DEU

Michuano ya mkondo wa kwanza ni Aprili 26 an 27 wakati ya marudiano ni Mei 3 na 4. Fainali itakuwa uwanjani San Siro mjini Milan Mei 28. Kwa uchambuzi zaidi kuhusu droo hiyo naungana na mwenzangu katika meza ya michezo Sekione Kitojo kwa njia ya simu, Kitojo, Hii ni mara ya kwanza kwa City kutinga nusu fainali ya dimba hili katika historia yao, unahisi wapinzani wao Real Madrid wanaweza kutumia faida ya uzoefu walio nao katika kutinga fainali?

Europa League

Katika droo ya Europa League, mabingwa watetezi Sevilla wa Uhispania wamepengwa dhidi ya Shakthar Donetsk ya Ukraine. Villarreal nao watakuwa na miadi na Liverpool katika nusu fainali ya pili.

Droo hiyo inaiweka hai nafasi ya kuwa na fainali ya timu zote za Uhispania kama tu ilivyokuwa katika mwaka wa 2012 wakati Atletico Madrid iliipiku Athletic Bilbao 3-0.

Mechi za nusu fainali ni Aprili 28 na Mei 5. Fainali ni mjini Basel Mei 18.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Yusuf Saumu