1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dresden:Merkel achaguliwa tena kukiongoza CDU

28 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoh

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amechaguliwa tena kwa wingi mkubwa wa asili mia 93, kukiongoza chama chake Christian Demokratik-CDU. Baada ya kuchaguliwa kwake katika mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho mjini Dresden, Bibi Merkel alisema,”Nimeukubali uchaguzi huu. Ninawashukuru kwa kunipa imani yenu na ninafuraha ya kushirikiana pamoja zaidi. Kwa moyo mkunjufu-Ahsanteni".Katika hotuba yake Bibi Merkel alitoa wito wa umoja na mshikamano chamani, chini ya kivuli cha upinzani unaozid dhidi yake, kutoka kwa Viongozi wa chama wa mikoa. Mmoja wao Waziri mkuu wa North Rhine Westphalia Jürgen Ruttgers alichaguliwa Makamu mwenyekiti kwa asili mia 58 ya kura.