1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC:Mapambano makali mjini Goma

20 Novemba 2012

Huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ripoti zinasema waasi wa kundi la M23 wameudhibiti uwanja wa ndege wa Goma.

https://p.dw.com/p/16m92
Mapigano karibu na uwanja wa Ndege wa Goma
Mapigano karibu na uwanja wa ndege wa GomaPicha: AP

Hali hii ni baada ya mapambano makali yanayoendelea kati ya waasi hao na vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na jeshi la Umoja wa mataifa.

Kupata zaidi juu ya hali ya mambo ilivyo Amina Abubakar amezungumza hivi punde na mbunge wa jimbo la kivu ya kaskazini, Mayombo Omary Bin Fikira na kwanza alimuuliza ikiwa anaweza kuthibitisha ripoti kwamba waasi wameuteka uwanja huo wa ndege wa Goma .

(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman