1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Waziri mkuu wa zamani Matata Ponyo aachiwa huru

15 Julai 2021

Mahakama ya Katiba nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imebatilisha uamuzi wake wa kumuweka waziri mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo kwenye kifungo cha nyumbani.

https://p.dw.com/p/3wWIZ
DR Kongo Ex-Premierminister Augustin Matata Ponyo
Picha: Florida Zantoto/Press Office Primeminister Kongo

Wakili wake Laurent Onyemba aliliambia shirika la habari la AFP kwamba waziri mkuu huyo wa zamani hayuko tena kizuizini na alirudi nyumbani kwake akiwa mtu huru bila ya kuandamana na polisi.

Uamuzi wa mahakama hiyo umetolewa siku moja tu baada ya bwana Ponyo kupewa kifungo cha nyumbani huku ukisubiriwa uchunguzi katika mashtaka ya ubadhirifu wa fedha yaliyokuwa yanamkabili.

Mnamo mwezi Mei waendesha mashtaka waliomba bunge kumwondolea kinga waziri mkuu huyo wa zamani Matata Ponyo ambaye sasa ni seneta ili aweze kuchunguzwa kuhusiana na madai ya ufisadi.

Soma pia: Baraza la seneti lamuondolea kinga Matata Ponyo

Lakini bunge la senetil ilipiga kura ya kupinga ombi hilo kwa sababu mahakama ya katiba nchini humo iliyotoa ombi hilo haina mamlaka ya kuwafungulia mashtaka wabunge.

Kesi za jinai zinazowakabili wabunge nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huwa zinasikilizwa kwenye mahakama maalum.