1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

CENI yaanza kuandikisha raia Mashariki mwa Kongo

Admin.WagnerD16 Februari 2023

Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Tume ya uchaguzi CENI imeanzisha leo zoezi la kuwaandikisha wapigakura katika majimbo ya mashariki, licha ya majimbo hayo kukabiliwa na changamoto za kiusalama.

https://p.dw.com/p/4NZwW
DRC Wählerregistrierung in der Region Nord-Kivu
Picha: Benjamin Kasembe/DW

Tangu mapema asubuhi raia wa Bukavu wamejitokeza na kufurika kwa wingi kwenye mistari mbele ya vituo mbalimbali vya usajili ili kupewa kadi mpya ya uchaguzi.

Tangu uchaguzi wa mnamo mwaka 2006, kadi ya uchaguzi inatumika kama kitambulisho kwa muda.

Prince Cinamula ni mkazi wa Bukavu ambaye tayari amepata kitambulisha cha kupiga kura,ambae alikisubiri kwa siku kadhaa, amesema ni muhimu kuzingatia wapiga kura wapya.

"Kitatusaidia pia kwa matumizi mengi ikiwemo hata kusafiri"

Alisema mpiga kura huyo ambae amepata nakala yake ya kitambulisho.

Zoezi la uandikishwaji linavyokwenda

Baada ya kuandikishwa wapigakura katika majimbo ya magharibi mwa Congo mnamo Desemba, na katika majimbo ya kusini na ya kati, hii ni zamu ya kusajiliwa kwa wapiga kura katika eneo la Kivu.

Kwa mujibu wa ratiba ya iliopangwa na tume ya uchaguzi CENI, likijumuisha majimbo saba ya mashariki ikiwemo pia Kivu kusini na jimbo la Kivu Kaskazini ambalo linakaliwa kwa sehemu moja na waasi wa M23.

 Eneo hili la tatu pia linahusu raia wa Congo wanaoishi ugenini nchini Canada na Marekani. 

Tume huru ya uchaguzi imehakikisha kwamba kila kitu kiko tayari kwa mchakato huo.

Soma pia:Changamoto za usajili wa wapigakura nchini Kongo

Paul Muhindo naibu msemaji wa tume ya uchaguzi, akiwa ziarani Kivu kusini, amesema kuna umuhimu kuhusu kuimarishwa ulinzi kwenye vituo.

"Tumekutana na gavana wa kivu kusini na ametuhakikishia kwamba polisi itatoa ulinzi wa vituo"

Alionengeza kuwa  CENI inaamini kwamba tuko tayari kuanza kuwaorodhesha wapigakura tkuanzia siku ya  alhamisi.

Raia wazungumzia suala la usalama

Wapigakura yapata milioni tatu wanatarajiwa baadha ya harakati hii itakayofanyika katika senta 921 za uorodheshaji katika jimbo la Kivu kusini. 

Demokratische Republik Kongo | symbolisches Wahllokal in Beni
Baadhi ya raia waliojitokeza kujiandikishaPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Lakini baadhi ya raia wametaka kwanza serikali ya Congo itiliye maanani suala la usalama mashariki mwa Congo, ambako kumeshuhudiwa mashambulizi ya mara kwa mara ya kushukiza.

Makundi yanayomiliki silaha na yale ya waasi ikiwemo kundi la M23, yamekuwa yakiendesha mashambulizi makali katika eneo hilo na kusababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine wakiyakimbia makaazi yao, kwa mujibu wa ripoti za kimataifa.

Itakumbukwa kwamba baadhi ya majimbo husika yanapatikana kwenye mipaka ya Congo na nchi jirani, tume ya uchaguzi imetoa onyo kwa wageni watakaothubutu kujipenyeza ili kujipatia kitambulisho cha kupiga kura.

Monusco yachangia kufanikisha zoezi hilo

CENI pia inahakikisha kwamba Ujumbe wa Kulinda amani wa umoja wa mataifa nchini Congo Monusco umechangia pakubwa kufanikisha zoezi hilo la kidemocrasia.

Monusco imefanikisha katika usafirishaji wa vifaa katika maeneo yasiofikika kirahisi kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara.

Maandamano ya kushinikiza amani DRC

Haya yanajiri wakati Rwanda inalituhumu jeshi la Congo kuwa limefyatua risasi usiku wa kuamkia jana jumatano kwenye mpaka wake wa Ruzizi ya pili mjini Bukavu.

Soma pia:Baadhi ya wakaazi wazuiwa kujiandikisha kama wapiga kura DRC

Gavana wa Kivu kusini na mkuu wa jeshi la FARDC kivu kusini wametupilia mbali tuhuma hizo wakisema Rwanda inataka kuleta mivutano kwa madai ya uongo, kama inavyofanya kwa vita vya uchokozi huko Kivu Kaskazini. 

Viongozi hao wanasema milio ya risasi iliosikika ni kati ya jeshi la Congo waliolinda mpaka huo na kundi la magenge wa Congo waliojaribu kuvamia ngome yao ili kujipatia silaha bila kufanikiwa, na kwamba hali imerudi kuwa shwari.