Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ubalozi wa China mjini Kinshasa umetoa wito kwa raia wote wa China kuondoka Kivu Kusini na mikoa jirani ya Kivu Kaskazini na Ituri kufuatia shambulizi lililo sababisha raia 5 wachina kutekwa nyara na polisi mmoja wa Congo kupoteza maisha Jumapili wakati kambi ya Wachina wachimba migodi iliposhambuliwa katika wilaya ya Fizi