1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yarejea katika kinyang'anyiro kwa kishindo

3 Februari 2020

Borussia Dortmumd wamepata tena nguvu zao za kutikisa nyavu. Wamefunga mabao 15 katika mechi zao tatu tangu Bundesliga iliporejea kitumua vumbi Januari. Nguvu hizo zimechangiwa pakubwa na makinda wawili

https://p.dw.com/p/3XDGs
Fußball Bundesliga Borussia Dortmund - Union Berlin Erling Haaland und Jadon Sancho
Picha: picture-alliance/RHR-FOTO/D. Ewert

Wakati mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland mwenye umri wa miaka 19 amegonga vichwa vya habari kwa mabao saba katika mechi zake tatu za kwanza katika Bundesliga, Jadon Sancho, Muingereza huyu amefanya kazi kubwa kuirejesha Borussia Dortmund katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa ligi.

Winga huyo wa England amefunga mabao tisa katika mechi zake tisa zilizopita katika Bundesliga, na akutoa assist saba zaidi katika kipindi hicho. Mabao hayo yalikuwa muhimu sana kwa Dortmund kupanda hadi nafasi ya tatu na pengo la pointi tatu dhidi ya vinara. Waliwapiga Union Berlin 5 – 0. Sancho ameonekana kuelewana viruzi na Halaand. Kinyang'anyiro cha Bundesliga kinawahusisha farasi wanne. Julian Brandt ni winga wa BVB. "Nadhani hauwezi kutegemea tutafunga mabao matano katika kila mechi sassa, hilo ni kweli. Lakini licha ya mabao tuliyofunga, ni muenendo mzuri kuwa sasa tunafungwa mabao machache kadri mechi zinavyoendelea. Tunaimarika katika vitu ambavyo hatukuvifanya vizuri katika nusu ya kwanza ya msimu na katika mashambulizi bado tuko hatari. Hilo ni jambo zuri."

1. Bundesliga 20. Spieltag | 1. FSV Mainz 05 vs. FC Bayern München | 3. TOR Bayern
Bayern wamewaondoa Leipzig usukani Picha: Getty Images/Bongarts/A. Grimm

RB Leipzig iliendelea kuyumba na kupoteza uongozi wao kileleni wa mwanya wa alama nne katika kipindi cha wiki mbili tu. Wamewapisha mabingwa Bayern ambao wanaongoza kwa pengo la pointi moja wakiwa na pointi 42. Leipzig walitoka nyuma na kulazimisha sare ya 2 – 2 na nambari nne Borussia Moenchengladbach. Kocha wao Julian Nagelsmann anasema kuyumba kwa timu yake sio kitu cha kawaida: "Kutoka nyuma na kufunga ni vizuri. Tulifanya hilo vizuri. Kulikuwa na shinikizo kubwa katika kipindi cha pili. Nadhani tulionyesha ukomavu kiakili katika kipindi cha pili na kuwawekea mbinyo. Pia tulifanya mabadiliko kwa kuwaweka washambuliaji wengi. Nadhani tulikuwa na washambuliaji watano au sita uwanjani baada ya hapo. Kwa hiyo nadhani ni sawa tuligawana pointi."

Bayern waliwapiga Mianz 3 -1  katika mechi ambayo mshambuliaji wake Robert Lewandowski alifunga bao lake la 22 msimu huu. Licha ya ushindi huo, kocha wa Bayern Hansi Flick hakufurahiswha na kiwango cha mchezo wa vijana wake "Tulishinda 3 – 1, tumeshinda mechi ya sita mfululizo. Tulipata nafasi tatu na tukafunga mabao matatu. Ilikuwa rahisi sana. Kisha labda tukapunguza kasi kidogo na ndio maana tukairejesha Mainz mchezoni kwa ushindi wa 3 – 1. Na tunajua kuwa kama bao la pili lingefungwa, nini kingefanyika hapa kwa watazamaji. Nna furaha sana kwamba tumeshinda mechi nsita mfululizo." 

Bayer Leverkusen wanamalizia nafasi ya tano bora kwenye ligi na pointi 34 baada ya kuzabwa na Hoffenheim 2 – 1.