Borussia Dortmund yaichapa Freiburg 3-1
24 Septemba 2016Dortmund ambao sasa imefunga mabao 14 katika mechi zao tatu za Bundesliga, walitakiwa kufunga kazi kitambo kabla Freiburg kukomboa dakika ya sitini ya mchezo na kuufanya mpambano huo kuwa mkali. Hata hivyo mikwaji ya Pierre-Emerick Aubameyang na Luksz Piszczek na bao la muda wa ziada lilitiwa wavuni na Raphael Guereiro liliiwezesha Dortmund kujihakikishia ushindi wa nne katiak mechi tano walizocheza msimu huu wa 54 wa ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani. Dortmund sasa imesawazisha rekodi ya kushinda mechi 24 ilizocheza nyumbani katika uwanja wa Signal Iduna Park bila kushindwa:
Dortmund sasa iko kileleni mwa ligi pamoja na mabingwa watetezi Byern Munich, zote zikiwa na pointi 12. Bayern inakabana koo na Hamburg SV Jumamosi (24.09.2016)
"Baada ya kuanza kwa udhaifu dakika 15 za kwanza, tulicheza vyema katika kipindi cha kwanza na tulitakuwa kuongoza kwa mabao zaidi," alisema kocha wa Dortmund Thomas Tuchel, ambaye timu yake ilikuwa imefunga mabao matano au zaidi katika mechi tatu zilizopita katika mashindano yote. "Baadaye mchezo ulibadilika ukawa mgumu" na tukababaika. Lakini inafurahisha tumefaulu kuondoa hofu, hususan baada ya ushindi mkubwa mara tatu mfululizo."
Huku Dortmund ikiajiandaa kuikaribisha nyumbani Real Madrid katika mchuano wa kombe la mabingwa Ulaya wiki ijayo, Tuchela aliongeza kusema, "Ufanisi huu umekuja wakati muafaka kabisa."
Mwandishi:Josephat Charo/rtre
Mhariri: Sekione Kitojo