1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund waelekea Marekani kwa kambi ya mazoezi

15 Julai 2019

Borrusia Dortmund wameondoka leo kwenda Marekani kwa ajili ya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya. BVB wanasafariri bila ya beki wao wa kati Abdou Diallo.

https://p.dw.com/p/3M6wb
Fußball Bundesliga Hertha BSC- Borussia Dortmund
Picha: picture-alliance/dpa/A. Gora

Borrusia Dortmund wameondoka leo kwenda Marekani kwa ajili ya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya. BVB wamesafiri bila ya beki wao wa kati Abdou Diallo ambaye anahusishwa na uhamisho wa kujiunga na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain.

Msemaji wa klabu hiyo ya Bundesliga amethibitisha habari hizo, na kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Diallo tayari yuko Paris kwa ajili ya vipimo vya matibabu.

Diallo mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Dortmund mwaka jana akitokea Mainz lakini anahofia kuwa baada ya kurejea kwa beki wa Ujerumani Mats Hummels huenda asipate nafasi nyingi za kucheza. Dortmund wana mabeki saba wa kati kikosini. Inakadiriwa kuwa PSG watatoa euro milioni 34 kumpata Diallo. BVB watakuwa Marekani kwa wiki moja ambapo watacheza na Seattle Sounders Alhamisi na kisha mabingwa  wa Champions League

Liverpool wanaoongozwa na kocha wa zamani wa Dortmund Juergen Klopp siku ya Jumamosi. Msimu wa Bundesliga unaanza katikati ya Agosti.