1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund na Köln waanza msimu vyema, Leipzig waguchia

8 Agosti 2022

Borussia Dortmund walifanya sajili zao mapema na kudaiwa kwamba ni mojawapo ya timu zilizojipanga vyema msimu huu na huenda wakawapa ushindani mkali Bayern Munich kwa taji la Bundesliga.

https://p.dw.com/p/4FGrg
Fussball Bundesliga | Borussia Dortmund - Bayer 04 Leverkusen
Picha: Bjoern Reichert/Jan Huebner/IMAGO

Wao walipata ushindi wa bao moja kwa bila walipokuwa wakicheza na bayer Leverkusen waliomaliza msimu uliopita katika nafasi ya tatu.

Nahodha Marco Reus ndiye aliyekuwa mfungaji wa goli hilo la pekee na kocha Edin Terzic alikuwa na haya ya kusema.

"Ndiyo ilikuwa mechi ngumu sana, na ni matumaini yetu kwamba tunaweza kuwalipa mashabiki wetu kwa mchezo mzuri. na baada ya muda cheche tulizokuwa tunazitaka kwenye mchezo zikajitokeza. Uwanja mzima ulitushabikia tulilazimika kujitahidi sana na kwa kweli mashabiki walisaidia sana," alisema Terzic.

1. FC Köln - FC Schalke 04
Wachezaji wa FC Köln wakisherehekea baada ya kufunga goliPicha: Marius Becker/dpa/picture alliance

Miamba wengine RB Leipzig ambao walimaliza msimu uliopita kwa kishindo, walianza msimu huu kwa kuguchia kidogo kwani walitoka sare ya bao moja na VfB Stuttgart, nyota wao Christopher Nkunku akiwafungia hilo goli lao.

FC Cologne walikuwa nyumbani kuwakaribisha vijana wapya Schalke 04 na wakawazima mori wao wa kupanda daraja kwa kuwachapa magoli 3-1.