Dola la Kiislamu lauwa watu zaidi ya 4,000 Syria tangu 2019
29 Juni 2024Matangazo
Katika ripoti yake shirika lenye kuangazia haki za binaadamu nchini humo limesema wengi wa waathiriwa ni wanajeshi, baadhi ya watu wenye utiifu kwa serikali na wapiganaji wanaoongozwa na Wakurdi, lakini idadi hiyo pia inahusisha raia 627.
Zaidi ya nusu ya walioathirika kwa idadi ya watu 4,085 walikuwakatika eneo la jangwa kubwa la Badia nchini Syria, ambalo linavuka nje ya viunga vya Damascus hadi mpakani mwa Iraqi.
Kundi la Dola la Kiislamu lilifanikiwa kuyateka maeneo makubwa ya Syria na Iraq mwaka 2014, na kutangaza kile kinachoitwa ukhalifa na baadaye mwaka huo Juni kuanzisha operesheni za kigaidi.