DOHA: Zawahri wa Al-Qaeda azionya Uingereza na Marekani
5 Agosti 2005
Naibu kiongozi wa kundi la Al Qaeda,Ayman al Zawahri ameonya kuwa mashambulio mengine yatafanywa nchini Uingereza na Marekani.Onyo hilo lilitolewa kwenye kanda mpya ya video iliyo onyeshwa na kituo cha televisheni cha kiarabu cha Al Jazeera.Katika kanda hiyo ya video,Zawahri amesema,mashambulizi yaliofanywa Julai 7 kwenye vyombo vya usafiri mjini London,yamesababishwa na siasa ya waziri mkuu wa Uingereza,Tony Blair kuhusu Iraq.Zaidi ya watu 50 waliuawa katika mashambulizi hayo.Zawahri ameionya Marekani vile vile kuwa itapata hasara zaidi ikiwa moja kwa moja haitohamisha majeshi yake kutoka Iraq.Tangazo la Zawahri limetolewa wakati ambapo polisi kwa maelfu wana operesheni kuu ya kulilinda jiji la London,baada ya treni tatu za chini ya ardhi na basi moja kushambuliwa na watu waliojitolea muhanga maisha,majuma manne ya nyuma.