1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Doha. Majeshi ya Ujerumani kuyapa mafunzo majeshi ya Iraq.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7B6

Majeshi ya Ujerumani Bundeswehr, yataendelea kutoa mafunzo kwa vikosi vya jeshi la Iraq nchini Abu Dhabi. Maafisa wa Ujerumani , Iraq na Abu Dhabi wametia saini makubaliano ambayo yatatoa nafasi kwa jeshi la Ujerumani kuwapa mafunzo wanajeshi 350 wa Iraq katika muda wa mwaka mmoja ujao.

Makubaliano hayo yametiwa saini pamoja na waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung, ambaye yumo ziarani katika eneo hilo.

Wakati huo huo , waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier yumo katika ziara ya siku tano katika mashariki ya kati. Hivi sasa yuko Misr akitarajiwa baadaye kwenda Israel na Palestina kabla ya kuhudhiria mkutano kuhusu Iraq mjini Instanbul.