1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Dissanayake avunja bunge Sri Lanka

25 Septemba 2024

Rais mpya wa Sri Lanka, Anura Kumara Dissanayake, amelivunja bunge la nchi hiyo na kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4l2zh
Dissanayake Sri Lanka
Rais Anura Kumara Dissanayake wa Sri Lanka.Picha: Rajesh Kumar Singh/AP Photo/picture alliance

Mwanasiasa anayefuata mrengo mkali wa kushoto, anatarajia kwamba hatua hiyo itaimarisha nafasi yake madarakani na kumuwezesha kutekeleza sera zake kikamilifu.

Akitangaza kupitia gazeti rasmi la serikali, Dissanayake amesema uchaguzi wa bunge utafanyika Novemba 14 mwaka huu, na vikao vya bunge hilo kuanza tarehe 21 Novemba.

Soma zaidi: Rais mteule wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake aahidi mabadiliko ya kiuchumi

Kiongozi huyo mpya mwenye umri wa miaka 55, alitangazwa mshindi wa uchaguzi siku ya Jumapili na kuapishwa siku ya pili yake, na kumchaguwa Harini Amarasuriya mwenye umri wa miaka 54 kuwa waziri mkuu.

Tayari ameziweka wizara za ulinzi, fedha na nishati chini yake. Muungano wa National People's Power, NPP, ambao ndio alioutumia kuchaguliwa una viti vichache bungeni.