Diego Costa aendelea kuwika Uingereza
30 Septemba 2014Edin Dzeko aliufumania mlango mara mbili wakati mabingwa Manchester City ikipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Hull City na kuchupa hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi , point mbili nyuma ya Southmpton , iliyoishinda Queens Park Rangers kwa mabao 2-1.
Manchester United imesogea katika nafasi ya saba ikiwa imepata ushindi wake wa pili msimu huu chini ya kocha Luis van Gaal kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United.
Arsenal na Tottenham Hotspurs , Liverpool na Everton ziliridhika na sare wakati mapambano ya watani wa jadi mjini London yakiishia kwa sare ya bao 1-1.
Nchini Uhispania , Barcelona na Real Madrid zimeendelea kufukuzana wakati timu zote hizo zikipata ushindi mwishoni mwa juma, ambapo Atletico Madrid haikuachwa nyuma ambapo iliiadhibu Seville kwa kuitwanga mabao 4-0.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / dpae / rtre , ZR
Mhariri: Iddi Ssessanga