1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DFB yazungumzia wafanyakazi wahamiaji Qatar kulipwa fidia

13 Januari 2023

Rais wa Shirikisho la Kandanda Ujerumani - DFB, Bernd Neuendorf anaamini kuwa shirka hilo lina wajibu wa kuwalipa fidia wafanyakazi wahamiaji nchini Qatar baada ya Kombe la Dunia.

https://p.dw.com/p/4M9dF
DFB-Pressekonferenz mit Bernd Neuendorf
Picha: Arne Dedert/dpa/picture alliance

Rais wa Shirikisho la Kandanda Ujerumani - DFB, Bernd Neuendorf anaamini kuwa shirka hilo lina wajibu wa kuwalipa fidia wafanyakazi wahamiaji nchini Qatar baada ya Kombe la Dunia. Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA, Gianni Infantino, aliwahakikishia kuwa malipo ya aina hiyo yanapaswa kutolewa, lakini Neuendorf amesema hawajui hasa ni vipi mpango huo utatekelezwa. Akizungumzia mada hiyo mjini Cologne, Rais huyo wa DFB alisema Kombe la Dunia la Qatar halipaswi kusahaulika na lengo la wadau kugeukia matukio mengine makubwa ya kandanda. Mashirika ya haki za binaadamu na vyama vya mashabiki vilidai kuwa FIFA ilipe mamilioni ya fedha katika kuwafidia wafanyakazi wahamiaji nchini Qatar.