DETROIT : General Motors kupunguza ajira
18 Oktoba 2005General Motors kampuni kubwa kabisa ya magari duniani imesema inapanga kupuguza ajira za watu 25,000 ifikapo mwaka 2008 katika marekebisho makubwa ya kuepusha hasara.
GM imesema pia imefikia makubaliano ya majaribio na chama cha wafanyakazi cha Marekani cha United Auto Workers ya kupunguza mabilioni ya dola katika huduma za afya kwa ajili ya wafanyakazi na wastaafu.Hatua hiyo inakwenda sambamba na tangazo la kampuni hiyo ya magari kutoka Detroit kwamba imepata hasara ya dola bilioni 1.6 katika kipindi cha robo mwaka cha mwaka huu.
Uongozi wa kampuni hiyo ya GM umesema lengo lake la jumla ni kupunguza gharama za dola bilioni tano kwa mwaka ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao.
Hata hivyo kampuni hiyo haikutowa maelezo ya kutosha juu ya uwezekano wa kufungwa kwa mitambo ya kuunganisha magari na ya vifaa vya magari.