Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mhimili wa siasa, uchumi na ushirikiano kati ya nchi za jumuiya hiyo. Kumekuwa na mvutano kutokana na tofauti ya mwelekeo wa kisiasa kwa nchi mwanachama. Bali lengo ni kufikia umoja wa kisiasa kati ya nchi mwanachama Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini. Nchi hizo zina mitazamo gani kuhusu demokrasia? Mohammed Abdul-Rahman ajadili katika "Maoni".