1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza afika Kibbutz Israel

23 Novemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Cameron ameutembelea mji wa Kibbuze uliolengwa katika uvamizi wa Oktoba 7 uliofanywa na wanamgambo wa Hamas uliosababisha watu 1200 kuuwawa.

https://p.dw.com/p/4ZN11
Israel Kibbuz Beeri 2023 | Besuch von David Cameron und Eli Cohen
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron akiwa na mwenzake wa Israel Eli CohenPicha: Alexander Ermochenko/REUTERS

Waziri mkuu huyo wa zamani wa Uingereza ambaye aliteuliwa wiki iliyopita kuwa waziri wa mambo ya nje,ameoneshwa maeneo kadhaa yaliyoharibiwa katika mji huo wa Kibuttz Be'eri.Ziara yake nchini Israel imekuja baada ya hapo jana kukutana na wenzake kutoka nchi za Kiarabu na za Kiislamu mjini London na kujadili kuhusu mgogoro huo kati ya Israel na Hamas.Cameron ameyapongeza makubaliano ya kusitisha vita kwa siku nne, kati ya serikali ya Israel na Hamas, akiyaita hatua muhimu na kuzitaka pande zote kuyatekeleza kikamilifu.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW