1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DARFUR. Wafadhili watoa ahadi na Koffi Annan yuko Sudan.

27 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF9b

Wafadhili wametoa ahadi ya takriban dola milioni mia tatu kuusaidia Umoja wa Afrika kupanuza kikosi chake cha kulinda amani katika jimbo la Darfur magharibi mwa nchi ya Sudan.

Maafisa wa Umoja wa Afrika wamesema kuwa Canada imetoa ahadi ya mchango mkubwa zaidi wa dola milioni 133 ikifuatiwa na Marekani ambayo imeahidi kutoa dola milioni 50.

NATO na Umoja wa Ulaya zitatoa msaada wa mikakati.

Hivi sasa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Koffi Annan yuko mjini Khartoum kuihimiza serikali ya Sudan irudie mazungumzo ya amani na waasi wenye silaha walio katika jimbo la Darfur.

Annan amesema kuwa anataka kuhakikisha tarehe ya kuanzishwa kwa mazungumzo hayo yaliyokwama mwezi Desemba imetolewa.