DARFUR. Pesa zahitajika kudumisha amani Darfur.
25 Mei 2005Matangazo
Shirika la chakula la umoja wa mataifa linataka dola milioni 62 zitolewe kwa dharura kulisaidia eneo la Darfur ikiwa kweli ulimwengu unataka amani idumishwe katika eneo hilo.
Kadri watu elfu 580 wanatarajiwa kurejea nyumbani huko Darfur baada ya msimu wa mvua ya masika, lakini hawana mahala kwa kwenda kwani makazi yao yalibomolewa wakati wa machafuko.
Fedha hizo zitatumiwa kununua mbegu, vifaa vya kilimo na kuijenga upya miundo mbinu katika eneo hilo.