1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM:Mustakabali wa uchaguzi wa Tanzania mashakani.

27 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEO4

Mamlaka zinazohusika na uchaguzi nchini Tanzania leo zimekuwa katika majadiliano ya uwezekano wa kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika siku ya Jumapili ijayo ya tarehe 30,baada ya kifo cha mgombea mwenza wa chama cha upinzani cha CHADEMA.

Mkutano wa dharura wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania umekuwa ukiendelea hadi jioni hii kujadili suala hilo.

Chini ya sheria za Tanzania,wagombea ni lazima wapitishwe na tume ya uchaguzi,kabla hawajapigiwa kura na majadiliano yanayoendela hivi sasa huenda yakatuama zaidi iwapo kuna muda wa kutosha kwa chama cha CHADEMA kutoa jina la mtu mwengine kuchukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na mgombea mwenza aliyefariki dunia.

Utata huo umekuja baada ya kifo cha Bwana Jumbe Rajab Jumbe,aliyekuwa mgombea mwenza kwa chama cha CHADEMA,aliyefariki dunia jana.