1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAR ES SALAAM: Migogoro ya Zimbabwe yatafutiwa ufumbuzi

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEM

Viongozi wa kusini mwa Afrika wamekusanyika Tanzania kuijadili migogoro ya kisiasa na kiuchumi ya Zimbabwe inayozidi kushika kasi. Wanadiplomasia wanasema viongozi hao wa Kiafrika katika mkutano unaoongozwa na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania,watajaribu kumuambia Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alie na umri wa miaka 80, kutogombea tena uchaguzi wa mwaka ujao.Mkutano huo unafanywa mjini Dar es salaam,siku moja baada ya polisi nchini Zimbabwe kuvamia makao makuu ya chama cha upinzani MDC na kuwakamata watu darzeni kadhaa.Polisi imesema,watu hao wamekamatwa kuhusika na uchunguzi unaofanywa kufuatia miripuko ya bomu ya hivi karibuni nchini Zimbabwe.Chama cha MDC kinalaumiwa kuhusika na miripuko hiyo.Mapema mwezi huu wanaharakati wa upinzani ikiwa ni pamoja na kiongozi wa MDC, Morgan Tsvangirai,walipigwa vibaya sana baada ya kukamatwa na polisi.Taarifa ya pamoja inatazamiwa kutolewa mwishoni mwa mkutano wa SADC mjini Dar es salaam.